WAHITIMU WA VYUO KUSAIDIA KATIKA UANZISHWAJI VIWANDA
SIDO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) wamesaini Mkataba wa Ushirikiano (MoU) ili kuhakikisha ujuzi unaopatikana kutoka kwa wahitimu haubaki kwenye mashelfu na badala yake unageuzwa kuwa bidhaa / huduma inayouzika sokoni na hivyo kusaidia katika mchakato wa uanzishwaji viwanda nchini.