MWONGOZO WA UENDESHAJI WA UKUZAJI WA KONGANO KUSAIDIA MAENDELEO YA VIWANDA NA UKUAJI WA UCHUMI

Mnamo tarehe 21 Novemba, 2019, SIDO imejiwekea rekodi kwa kuingia hatua muhimu baada ya kupitisha "Mwongozo wa Uendeshaji wa Ukuzaji wa Kongano." Mwongozo huu ulitengenezwa kwa msaada wa zaidi ya wadau 200 kutoka serikalini na serikali za mitaa, sekta binafsi, wasomi na mashirika wa maendeleo, walioungwa mkono na Shirika la Kimataifa la Japan (JICA).

Kongano  hufafanuliwa kama Kongano ni mkusanyiko wa watu wanaofanya kazi zinazofanana au kushabihiana katika eneo moja au sehemu tofauti. Nchini Tanzania, Njia ya Ukuzaji wa kongano una dhumuni la  kuendesha maendeleo  ya viwanda kwa kutumia fursa  zilizopo ndani ya kongano zikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wadau mbali mbali kwenye minyororo ya thamani na kuhamasisha ushirikiano bainai yao. Kwa kuwa karibu na kushirikiana itasaidia katika upataji na usambazaji wa taarifa mbalimbali ambazo ni chanzo cha uvumbuzi.

SIDO imekuwa kichocheo kikubwa katika uendelezaji wa kongano tangu 2006, kwa msaada wa JICA na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Sweden (Sida). Kutokana na misaada hiyo kwa SIDO na wadau wengine, idadi ya wajasiriamali wanaozalisha mchele na alizeti hasa Mbeya uliongezeka kwa asilimia 85% kutoka 2010 hadi 2015. Kutokana na utafiti uliofanyika hivi karibuni katika mkoa wa Mbeya, Mwanza na Singida, kumekuwepo ongezeko la thamani kwa wana kongano kwa  asilimia 18-22% kutoka 2015 hadi 2018,  

Mnamo tarehe 14 na 15 Novemba, 2019, SIDO iliandaa semina Morogoro  wa kuandaa toleo maarufu (= muhtasari ) wa  mwongozo wa kongano.  Jumla ya  washiriki katika semina hiyo walikuwa 26 ambao walitoka maeneo mbalimbali  zikiwemo ofisi za RAS – Morogoro, SIDO mikoa (Dar es Salaam, Dodoma, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Singida Tanga, Morogoro  na SIDO HQ) na  wajumbe toka taasisi za  TCCIA-Morogoro , LIC na JICA, na mshauri wa maswala ya kongano.

Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo, aalifungua semina hiyo. Alisisitiza umuhimu wa wajasiriamali na maendeleo ya kongano katika kuleta maendeleo ya viwanda, na kuhimiza washiriki kuandaa mwongozo rafiki kwa watumiaji. Warsha hiyo ilijadili muundo na yaliyomo katika toleo hilo maalumu kupitia kazi za kikundi na majadiliano kwa jumla.

Toleo maarufu katika lugha ya Kiswahili litasaidia kuhamasisha maafisa wa juu na umma kwa ujumla. Zaidi  itasaidia watekelezaji wa mwongozo kwa uharaka. Uzinduzi wa toleo hili  maarufu umepangwa kufanyika mapema 2020.