SIDO YAKARIBISHA BODI MPYA YA WAKURUGENZI

Mnamo Oktoba 2018 Raisi wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli, alimteua  Profesa Elifas Bisanda,  ambaye pia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Open University, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SIDO.  Kufuatilia uteuzi huu, wanachama wengine waliochaguliwa kwenye Bodi ya SIDO ni Maduka Paul Kessy (Katibu wa Mkoa wa Dodoma), Profesa Bashira Alli Majaj (Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Seraphia Robert Mgembe (Mratibu wa Programu ya Kuimarisha Mali na Biashara - Mkurabita), Mhandisi Peter Chisawilo (Afisa Mtendaji Mkuu - Intermech Engineering Ltd), John Cheyo (Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) na Mhandisi Gilman Kasiga (Mkurugenzi wa Maendeleo na Biashara katika General Electric - GE) ambayo itatumika kwa miaka mitatu tangu uteuzi wao ulipofanyika  tarehe 3 Februari, 2019.

Mnamo  tarehe 11 Machi 2019, kwa mara ya kwanza, wajumbe waliochaguliwa walikutana na wajumbe wa menejimenti ya SIDO katika ukumbi wa SIDO Mkuu  kwa utambulisho na walipewa maelezo mafupi kuhusu shughuli zilizofanywa na SIDO katika kuendeleza Viwanda Vidogo na vya Kati nchini.  Utambulisho huu  ukifuatiwa na ziara ya  wajumbe wote kutembelea mtaa wa viwanda uliopo SIDO- Vingunguti  ambapo walijionea  shughuli mbalimbali zilizofanywa na wajasiriamali waliopanga  katika majengo ya SIDO – DSM.