Katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali za kupambana na virusi wa COVID – 19, Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limeunga mkono juhudi za serikali la kupambana na janga hili lililoikumba dunia ikiwemo Tanzania linaisha kwa kutoa elimu mbalimbali za kujikinga na virusi vya corona kwa kunawa mikono kila mara kwa sabuni na maji yanayotiririka, kutoshika maeneo ya pua, mdomo na macho. SIDO imeweza pia kutengeneza vitakasa mikono (sanitizer), sabuni za mikono pamoja vifaa vya kunawia mikono (ndoo za maji). Vifaa hivi vimetengenezwa kiutaalamu ambapo mtumiaji atatumia kirahisi bila ya kufungua koki za maji au sabuni. Ndoo Vifaa vina sehemu ya kukanyaga ili kuweza kutoa sabuni na pia maji bila kushika kwa mikono.
Jitihada hizi zinafanywa na mikoa mbalimbali ya SIDO ikiwemo Dodoma, Kilimanjaro, Singida, Dar Es Salaam, Kagera, Arusha, Iringa na Tanga. Wateja mbalimbali wamekuwa wakijitokeza na kutoa zabuni yakiwemo mashirika , taasisi mbalimbali za serikali, watu binafsi na taasisi za fedha.
Mjasiriamali, Bw. Kapalata ambaye ni mhitimu wa program ya kulea ubunifu, (kitamizi) inayoendeshwa na SIDO – Dar es Salaam nae hakukubali kubaki nyuma hivyo alikuja na ubunifu wa aina yake ambapo ametengeneza mashine ya kutakasa mwili mzima (sanitizing buuth). Mashine hiyo ina eneo la kuingilia na la kutokea. Moshi huanza kutoka kwenye mashine hiyo mara mtu akikanyaga eneo la kuingilia na hivyo kuzidi kusambaa mwilini mwake hadi atakapotokea upande wa pili. Mashine hii imekuwa kivutio kikubwa kwa waliyoiona na uhitaji kwa baadhi za hospitali na mabenki n.k kutokana na uwezo na utendeaji kazi wake.
Pia mjasiriamali George Buchafwe aliyeko eneo la Viwanda SIDO - Dar Es Salaam amekuja na dawa ya kujifukiza inayoitwa BUPIJI, ambayo imeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia watu wanaopata matatizo ya kushindwa kupumua vizuri, kuumwa kichwa na kukohoa. Dawa hiyo imejinyakulia umaarufu baada ya kuponya watu wengi waliyoitumia kwa kufuata maelezo yaliyotolewa. Sambamba na hili, mjasiriamali George ameweza pia kutengeneza mashine ya mvuke, Sauna, ambayo ameiweka dawa hiyo na hivyo mgonjwa huingia ndani ya mashine hiyo huku akiwa anavuta mvuke wenye dawa ya BUPIJI iliyowekwa kitaalamu. Baadhi ya mashine hizi zimechukuliwa na vituo vya afya ikiwemo hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa kwa ukaribu zaidi.
SIDO inaendelea na kutoa huduma zake zikiwemo za uweseshaji wazalishaji bidhaa na vifaa vinavyotumika kujikinga na virusi vya corona kwa kutoa ushauri wa kitaalamu, kuzalisha kwa kuzingatia vigezo na masharti ya ubora na kupata nembo ya alama za ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)