Maonesho ya Kimataifa ya Zimbabwe
01 Apr, 2026 10:00AM - 06:00PM Bulawayo - Zimbabwe

TANGAZO LA KUSHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BULAWAYO – ZIMBABWE

Wajasiriamali na wafanyabiashara mnaalikwa kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Bulawayo – Zimbabwe yatakayofanyika kuanzia tarehe 20/04/2026 hadi 25/04/2026 katika jiji la Bulawayo, Zimbabwe. Maonesho haya yanatarajiwa kuhudhuriwa na kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maonesho haya ni fursa muhimu ya kutafuta masoko na wateja wapya ndani ya Afrika, hususan nchini Zimbabwe, pamoja na kukuza biashara, kujifunza teknolojia mpya za uzalishaji na kujenga mtandao wa kibiashara na washiriki kutoka nchi mbalimbali.

Gharama za ushiriki zitajigharamia mshiriki mwenyewe. Kwa maelezo zaidi na taratibu za usajili, wasiliana na TANTRADE kupitia namba 0733 002 014. Karibuni sana kutumia fursa hii kukuza biashara na bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa.

Maonesho ya Kimataifa ya Zimbabwe
Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo