Upatikanaji wa Teknolojia

Upatikanaji wa teknolojia ni moja ya huduma ambazo SIDO inatoa ili kuhakikisha wajasiriamali wanapata teknolojia ya mashine ili kuanzisha na kukuza viwanda vyao. Mbinu zinazotumika kupata mashine za SMEs ni pamoja na; uzalishaji wa mashine kupitia Vituo vya Maendeleo ya Teknolojia vya SIDO (TDCs), karakana binafsi, taasisi za Utafiti na uboreshaji zinazozalisha teknolojia na kuwaunganisha na waagizaji wa mashine kutoka nje ya nchi. Vituo vya Maendeleo ya Teknolojia vya SIDO (TDCs) ni vituo vinavyomilikiwa na SIDO vya kusanifu na kutengeneza mashine mbalimbali na vipuri na utoaji wa huduma za uhandisi viwandani. TDCs ziko katika mikoa ya Lindi, Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Kigoma na Shinyanga. Wajasiriamali huweka oda zao kwa TDCs kutengeneza mashine au vifaa kwa ajili yao.

Karakana kibinafsi ni karakana ambazo zinamilikiwa na makampuni ya kibinafsi.  SIDO hutoa ushauri, mafunzo na kuwa na mashirikiano na karakana hizo ili kuchangia upatikanaji wa teknolojia kwa wajasiriamali.   Karakana hizi zinasaidia zaidi katika maeneo ambayo SIDO haina Vituo vya Maendeleo ya Teknolojia. Taasisi za R&D ni taasisi za Serikali zinazofanya utafiti, maendeleo, uvumbuzi, na kuzalisha teknolojia na vifaa mbalimbali vya mashine. Hizi ni pamoja na TEMDO, CAMARTECH, TIRDO, TDTC. Waagizaji na wauzaji wa mashine na vifaa ni makampuni ya kibinafsi ambayo yanaweza kuagiza mashine na vifaa ambavyo havipatikani nchini.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo