Imewekwa: 20 Jun, 2026
Vijana wapatao 60 kutoka halmashauri za wilaya za Tanga, Muheza na Mkinga wamehitimu mafunzo ya usindikaji wa vyakula yaliyolenga kuwawezesha kupata ujuzi wa kuongeza thamani ya mazao na kujiajiri kupitia shughuli za ujasiriamali.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na mradi wa East African Crude Oil Pipeline (EACOP) na kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya Sheria Kiganjani na SIDO.

