CRDB BANK NA SIDO TANGA ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA KUWEZESHA WAJASIRIAMALI
Imewekwa: 01 Sep, 2026
CRDB BANK NA SIDO TANGA ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA KUWEZESHA WAJASIRIAMALI

Meneja wa CRDB Bank, Bw. Elias Lugola, pamoja na Meneja Mahusiano wa Benki, Bi. Beatrice Mtewele, wametembelea Ofisi ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Tanga kwa lengo la kujitambulisha na kujadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo katika kuwawezesha wajasiriamali.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili fursa mbalimbali za ushirikiano zitakazowezesha SIDO na CRDB Bank kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi na kuwaunganisha na huduma za kifedha, hususan mikopo inayotolewa kupitia ushirikiano wa taasisi hizo.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuimarisha uratibu katika kuwabaini wajasiriamali wenye sifa za kupata mikopo, kuwajengea uwezo wa kuboresha biashara zao na kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kifedha.

Ushirikiano huo pia unalenga kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wajasiriamali, kukuza biashara zao, kuongeza uzalishaji na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo na za kati katika Mkoa wa Tanga

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo