Imewekwa: 15 Oct, 2025
Kutakuwa mafunzo ya ujasiriamali yatakayoendeshwa na Mhandisi Bi. Betty Rweabura siku ya Jumamosi tarehe 18/10/2025. Mafunzo hayo yameandaliwa na Bathel Chapel International na yatafanyikia katika ukumbi wa ofisi hiyo uliopo Mikocheni B, Barabara ya 26 ya Mwenda - DSM. Mafunzo hayo yataanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana. Yatahusiana na maswala ya uanzishaji wa viwanda, ubunifu kwenye biashara, masoko na utangazaji na masuala ya mashine na vifaa mbalimbali.

