Katika jitihada za kukuza wajasiriamali wa ndani na kuwafungulia masoko ya kimataifa, SIDO Mbeya iliweza kutoa huduma mbalimbali kwa mjasiriamali Naomi Mwasambili Mjasiriamali Naomi alipata fursa ya kushiriki maonesho ya Fruit Logistica yaliyofanyika katika mji wa Berlin nchini Ujerumani. Bidhaa alizopeleka kwenye maonesho ni aina mbalimbali za Chocolate kama vile milk chocolate, dark chocolate ambazo zimewekwa moringa, tangawizi, chia seed, macadamia, zabibu na korosho. Aliweza kushiriki maonesho haya chini ya taasisi ya Copra ambayo inasimamia mazao Tanzania. Akiwa ujerumani aliweza kukutana na balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Hassan Mwamweta. Bidhaa zake zilifurahiwa sana na hivyo kupata oda nyingi.
Huduma alizopata SIDO ni pamoja na kumsaidia katika kuanzisha kiwanda hicho; kumpatia mafunzo ya usindikaji wa vyakula na usimamizi wa biashara; kumsaidia katika kupata alama ya ubora wa bidhaa zake na kumwezesha kupata mikopo kupitia mifuko ya SANVN na CGS.

