Mheshimiwa Joel Nanauka, Mbunge wa Mtwara Mjini na Waziri wa nchi ofisi ya Raisi, Maendeleo ya Vijana wamefanya kikao na wadau mbalimbali kutoka mkoani Mtwara ili kutekelezaji mipango ya serikali kutimiza ahadi zake walizozitoa kipindi cha uchaguzi. SIDO ya Mkoa wa Mtwara kama mdau mmojawapo, imedhamiria kutekeleza shughuli zake sambamba na mipango hiyo.
Shughuli na jitihada hizo za SIDO zitajielekeza katika kusaidia makundi mbalimbali ya vijana na wanawake kuanzisha viwanda vidogo katika sekta za vipaumbeule ili kutengeneza ajira na kuboresha hali ya uchumi wa vijana wa mkoa wa Mtwara na wananchi kwa jumla.
Baadhi ya maeneo hayo ya kimkakati ni sekta ya uzalishaji, kilimo, biashara, uchumi wa bluu, ajira za kidigitali, utalii na usafirishaji. SIDO imejipanga kuyatekeleza hayo kupitia huduma zake kuu nne ambazo ni ubunifu wa uendelezaji teknolojia mbalimbali za mashine za kuongezaji thamani mazao ya kilimo na mifugo ambazo zitasaidia katika uanzishwaji na uendelezaji wa Viwanda. Huduma nyingine ni mafunzo ya biashara na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali; upatikanaji wa masoko na namna bora ya ufungashaji wa bidhaa ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko; upatikanaji wa maeneo ya pamoja ya uwekezaji kwa mkakati wa kongani za viwanda kwa walengwa wa makundi ya vijana na wanawake; utoaji wa mitaji midogo na mikubwa kupitia mifuko mbalimbali ya kutoa mikopo.. #PamojaTujenge Viwanda#

