NMB FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UBANGUAJI BORA WA KOROSHO - KILWA
Imewekwa: 17 Oct, 2025
NMB FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UBANGUAJI BORA WA KOROSHO - KILWA

Hivi karibuni, SIDO Lindi kwa ufadhili wa  NMB Foundation ilitoa  mafunzo ya siku 5 kwa wabanguaji  wa korosho kwa washiriki 50 toka wilaya ya Kilwa.

Lengo  kuu la mafunzo haya ni kutimiza adhma ya serikali ya kuongeza thamani zao la korosho. Wakulima na wazalishaji wengi wa korosho wamekuwa wanauza korosho kwenye magala au kwa kampuni kubwa zikiwa bado hazijaongezwa thamani. Hii imekuwa inawaumiza wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwa  faida yake ni ndogo ukilinganisha na korosho iliyobanguliwa.

Mafunzo haya yamewezesha wazalishaji hawa 50 kubangua korosho zenye ubora ambazo  zinakubalika ndani na nje ya nchi.   Baada ya mafunzo haya, kulikuwepo kwa kongamano kubwa la wadau wote wa korosho wakiwemo wamiliki wa magala, wazalishaji wa kati na wakubwa na watengeneza mashine mbalimbali za kusindika korosho.  

Katika kongamano hilo, Bodi ya korosho Tanzania iliwahakikishia wabanguaji wadogo kuwa,  watapata upendeleo  na kibali cha kununua korosho ghafi toka kwa wakulima bila kwenda kwenye mnada na pia wataunganishwa na wabanguaji wa kati na wakubwa kwa ajili ya masoko ya bidhaa zao ndani na nje nchi.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo