NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA APONGEZA USHIRIKI WA WAJASIRIAMALI BANDA LA SIDO
Imewekwa: 05 Jul, 2026
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA APONGEZA USHIRIKI WA WAJASIRIAMALI BANDA LA SIDO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,  Bw. Aristides Mbwasi, ametembelea Banda la SIDO katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF 2026) na kupongeza ushiriki mkubwa wa wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Akiwa ameambatana na viongozi wa SIDO, alijionea bidhaa na mashine mbalimbali za uongezaji thamani, zikiwemo za kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na bidhaa za vyakula, dawa za asili, nguo, sabuni na vipodozi vya asili. Aliipongeza SIDO kwa mchango wake katika kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo nchini.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha vifungashio vya bidhaa, kuwaunganisha wajasiriamali na masoko pamoja na taasisi nyingine za maendeleo ya biashara, na kuangalia namna ya kuwasaidia wajasiriamali wenye uhitaji wa mashine, hususan wenye ulemavu kupitia programu za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Pia aliwapongeza wajasiriamali wanaozalisha bidhaa za asili, akieleza kuwa matumizi ya malighafi za ndani yanachangia ukuaji wa uchumi na kuboresha afya na ustawi wa jamii.

 

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo