KATIBU MKUU AHIMIZA WAJASIRIAMALI KUSHIRIKI MAONESHO
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) limeandaa Maonesho ya 5 ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Magufuli Kahama- Shinyanga. Maonesho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 24 Oktoba 2026 na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Judith Kapinga (MB) na yataendelea hadi tarehe 30 Oktoba 2026.
Katika Maonesho hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum alikuwa mmoja wa wageni waheshimiwa waliotembelea mabanda ya wajasiriamali. Alipat fursa ya kujionea bidhaa bora zilizotengenezwa na kufurahishwa na ubunifu mzuri unaofanywa na wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Wakati wa ziara yake kwenye baadhi ya mabanda ya wajasiriamali, Katibu Mkuu alisisitiza kuwa, serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa SIDO inaendelea kuleta mapinduzi kwa wajasiriamali nchini. Alibainisha kuwa, hili linafikiwakupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo, ikiwemo upatikanaji wa teknolojia, mafunzo ya ujasiriamali, na kuwaunganisha wajasiriamali na masoko ya ndani na nje ya nchi.
Aidha aliongeza kuwa, lengo la maonesho siyo kuuza bidhaa pekee, bali pia kuwapa wananchi fursa ya kujifunza mbinu mpya za ujasiriamali na namna ya kuongeza kipato kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana.

