Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa uzalishaji wa mpunga. Shughuli za usagaji wa mpunga huzalisha kiasi kikubwa cha pumba za mpunga ambazo mara nyingi hutupwa au kuchomwa bila mpangilio. Hata hivyo, mabaki haya yana uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati safi ya kupikia kupitia teknolojia ya briquettes au gesi ya biomas. SIDO kupitia kituo cha kuendeleza teknolojia kilichopo Mbeya (TDC), kimekuja na teknolojia ya kuongeza thamani pumba za mpunga ili kupata nishati safi ya kupikia.
Hivi karibuni SIDO Mbeya ilifanya makabidhiano ya mashine ya uongezaji thamani pumba za mpunga mbele ya mgeni rasmi Afisa Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Bi. Devota Chacha akiwa anamwakilisha Afisa Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Mashine hiyo ilifadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia UNIDO ambapo itakayotumika kutengeneza kuni bora ambazo pia zitapunguza gharama za nishati, kulinda mazingira, kupunguza uchafuzi wa hewa, na kutoa fursa za ajira kwa vijana
SIDO Mbeya inawaajibu wa kusimamia kiwanda hiki ili teknolojia hii iweze kusaidia viwanda vingine vinavyojihusisha na uchakataji wa zao la mpunga. Ubadilishaji pumba za mpunga kuwa nishati safi ya kupikia ni suluhisho bunifu litakalochangia maendeleo endelevu; kuchochea uchumi wa nchi, kulinda mazingira na kuboresha afya za watumiaji. Kwa kuwekeza katika teknolojia hii, jamii zinaweza kupata chanzo cha nishati nafuu, salama na rafiki kwa mazingira.

