Imewekwa: 23 Jan, 2026
Hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Mhand. Prof. Sylvester Mpanduji alizindua mradi wa Inclu-Cities chini ya Proram ijulikanayo kama SASA. Mradi huu unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na kusimamiwa na Enabel. Lengo ni kusaidia biashara na shughuli zinazotunza mazingira hasa katika Wilaya ya Ilemela na Nyamagana. SIDO Mwanza inatekeleza mradi huu kwa kuwafikia wajasiriamali 230 ambao wanajishughulisha na ufugaji wa samaki kupitia vizimba, wasindikaji wa samaki na wale wote wanaojishughulisha na shughuli za kuhifadhi na kulinda mazingira.

