Imewekwa: 04 Jun, 2025
Washiriki wa mafunzo kutoka Kijiji cha Sukenya, Wilaya ya Ngorongoro wakiwa katika picha za matukio mbalimbali wakati wa mafunzo. Mada zilizotolewa ni Mpangilio wa kiwanda, Usafi na Usalama wa usindikaji wa Asali ambazo zilifundishwa na mkufunzi kutoka SIDO Arusha Mhand. Stephano Leyan. Lengo la mafunzo ni kuwapa ujuzi wa kusindika Asali ili kuongeza thamani mazao ya nyuki kwa ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali liitwalo FOTZ.

