SIDO IRINGA YAENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI
Imewekwa: 01 Sep, 2026
SIDO IRINGA YAENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI

Katika kuendelea kutekeleza jukumu la kuendeleza viwanda vidogo na kuwawezesha wajasiriamal nchini, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo mkoa wa Iringa imetembelea Verdat Clean Energy, kiwanda  cha kutengeneza nishati safi, kilichopo Mafinga kinachomilikiwa na kuendeshwa na vijana.

Ziara hiyo imelenga kutoa ushauri wa kitaalamu katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji, uendeshaji na uendelezaji wa biashara, pamoja na kutathmini fursa na changamoto zinazoweza kusaidia kiwanda hicho kukua, kuongeza tija na kuimarisha ushindani katika soko.

Kupitia ziara na huduma za aina hii, SIDO inaendelea kuwawezesha vijana kupata maarifa, ushauri na mbinu bora za uzalishaji na uendeshaji wa biashara, hatua inayochangia kujenga msingi imara wa viwanda vinavyomilikiwa na vijana.

SIDO inaendelea kuamini kuwa vijana ni nguvu kazi muhimu katika ujenzi wa uchumi shirikishi unaotegemea uzalishaji na viwanda. Kwa kuwawezesha vijana kutumia fursa zilizopo, kuendeleza ubunifu na kuongeza thamani ya bidhaa, juhudi hizi zina mchango katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo Tanzania 2050.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo