SIDO MTWARA YAWEKA MKAKATI WA UANZISHAJI KONGANI KATIKA KILA WILAYA
Imewekwa: 18 Feb, 2026
SIDO MTWARA YAWEKA MKAKATI WA UANZISHAJI KONGANI KATIKA KILA WILAYA

Katika jitihada za Serikali kuwezesha wananchi kiuchumi na kuongeza ajira kwa vijana, wanawake na makundi ya mahitaji maalumu, Serikali  ya awamu ya sita katika moja ya vipaumbele vyake,  imeanzisha kongani za Viwanda. Hii ni katika kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vidogo  na vya kati na  kuongeza ajira.

Katika kutekeleza hayo, Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara alikutana  na Katibu Tawala wa  Mkoa, Bi Bahati Geuzye,  ili kujadili namna ya kupata maeneo ya kongani za viwanda katika kila Wilaya ambapo wajasiriamali wataozalisha bidhaa mbalimbali watawekwa pamoja. Hii itarahisisha katika utoaji wa huduma mbalimbali za  kuboresha uzalishaji, utengenezaji wa bidhaa bora,  na uongezaji ajira zaidi kwa vijana na wananchi wa Mkoa wa Mtwara

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo