SIDO YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA 2026
Imewekwa: 17 Jun, 2026
SIDO YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA 2026

Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) linashiriki Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2026.

Katika banda la SIDO, wageni mbalimbali wameendelea kutembelea na kupata elimu kuhusu huduma na fursa zinazotolewa na shirika. Miongoni mwa wageni waliotembelea banda hilo ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, George Stanslaus Wambura, ambapo kulifanyika majadiliano kuhusu namna ya kuwajengea wafungwa uwezo wa ujasiriamali ili waweze kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao.

SIDO inawakaribisha watumishi wa umma na wananchi wote kutembelea banda lake ili kujifunza kuhusu fursa mbalimbali za ujasiriamali, uanzishaji wa viwanda vidogo, na matumizi ya malighafi zinazozalishwa nchini kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo