Imewekwa: 04 Jun, 2025
SIDO imeendelea kutoa huduma zake kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ikiwemo kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali. Kupitia maonesho yanayoandaliwa na SIDO na wadau mbalimbali bidhaa za wajasiriamali zimekuwa zinapata masoko ndani na nje ya nchi. Kwa mwaka huu 2025, wajasiriamali wapatao 135 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani wameweza kushiriki katika Banda la SIDO kwenye maonesho ya 49 ya kibiashara Tanzania yanayojulikana kama “Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam (DITF)” 2025

