SIDO TANGA YATEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA YA ASILI PANGANI
Imewekwa: 08 Sep, 2026
SIDO TANGA YATEMBELEA KIWANDA CHA MBOLEA YA ASILI PANGANI

Wataalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Tanga wamefanya ziara katika kiwanda kidogo kinachozalisha mbolea ya asili inayotokana na makumbi ya nazi.

Kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Pangani kinazalisha bidhaa inayojulikana kama Cocopeat, inayotokana na mabaki ya maganda ya nazi na kutumika katika shughuli mbalimbali za kilimo.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uzalishaji, kuongeza ufanisi pamoja na kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi viwango vya ubora vinavyohitajika ili kupata ithibati ya ubora.

Katika ziara hiyo, wataalamu wa SIDO walitoa ushauri kuhusu maboresho yanayoweza kufanyika katika mchakato wa uzalishaji na kuhakikisha ubora wa bidhaa unaimarishwa kwa kuzingatia mahitaji ya soko na viwango vinavyotakiwa.

SIDO inaendelea kuwa karibu na wajasiriamali na viwanda vidogo nchini kwa kutoa ushauri wa kitaalamu, kukuza ubunifu, kuendeleza teknolojia na kuongeza thamani ya malighafi zinazopatikana nchini. Juhudi hizo zinalenga kuimarisha ushindani wa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vidogo, kuongeza fursa za kiuchumi na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

SIDO – PAMOJA TUJENGE VIWANDA

 

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo