Kamishna wa Huduma za Urekebu ndani ya Jeshi la Magereza Tanzania na Uwezeshaji Kiuchumi, Bi. Amina Jumanne Kavirondo, alitembelea Banda la SIDO katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), 2026 ambapo alipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Vituo vya kuendeleza Teknolojia za SIDO pamoja na bidhaa mbalimbali zinatotengezwa na wajasiriamali wanaonufaika na huduma za SIDO.
Katika ziara hiyo, alipewa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na SIDO katika kukuza ujasiriamali, kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, pamoja na kuhamasisha uongezaji thamani wa mazao na bidhaa za ndani ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la ndani na nje ya nchi.
Alizungumzia kuhusu kuzidisha mashirikiano hasa katika kuwawezesha wafungwa kiuchumi ili pindi wanavyomaliza kutumikia vifungo vyao waweze pia kuendelea na ujuzi ambao watakuwa wameupata wa kutengeneza vitu mbalimbali.

