SHIRIKA LA MAENDELEO LA TIKA LAAHIDI  MASHINE ZA UCHAKATAJI KWA WAJASIRIAMALI
Imewekwa: 03 Mar, 2026
SHIRIKA LA MAENDELEO LA TIKA LAAHIDI  MASHINE ZA UCHAKATAJI KWA WAJASIRIAMALI

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO) katika mkoa  wa Dar es salaam imepokea ugeni wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA), Mr. Halim Omer Sogut. Huu ni muendelezo wa majadaliano baina ya SIDO DSM na Shirika la TIKA ambayo yamekuwa yakifanyika katika Ofisi za TIKA kwa lengo la kuwa na Mashirikiano.

Shirika la Maendeleo la TIKA limekuwa likiweka Mipango na Fedha kwa ajili ya kusaidia na kuwezesha tasnia ya ujasiriamali nchini kwa kipindi kirefu ili kuhakikisha wakina mama na Vijana wanajikwamua kiuchumi. Misaada hiyo imekuwa ikilenga kukarabati miundombinu, kuwezesha mashine na teknolojia mbalimbali za usindikaji, Programu za Nishati safi na miradi mbali mbali ya maendeleo.

Katika Ziara yake Mkurugenzi Mkazi, alipata wasaaa wa kutembelea Mtaa wa Viwanda wa SIDO - DSM, kutembelea jengo la usindikaji la KOICA, jengo la ushonaji pamoja na kujionea mafunzo ya utengenezaji wa Sabuni na Vipodozi yaliyokuwa yanaendelea.

Katika Ziara hiyo Kaimu Meneja wa Mkoa, Bw Jonathan Mbailuka, alipata wasaa wa kumueleza jitihada za Shirika katika kuendeleza tasnia ya ujasiriamali na uanzishwaji wa viwanda vidogo katika Mkoa wa Dar es salaam. Aidha ameeleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo miundombinu ya mafunzo ambaye imechakaa na mashine ndogo ndogo za uchakataji wa bidhaa.

Akijibu maombi ya Kaimu Meneja, Ndugu Omer ameahidi kusaidia Shirika katika kutatua changamo hizo na amekubali kufanya ukarabati wa madarasa na kusaidia katika kuwezesha mashine za kufundishia

Sambamaba na hizo amekubali kusaidia vikundi  mbalimbal vya wanawake na vijana  kwa kuvipatia mashine zenye thamani ya takribani million 70 zikiwemo mashine za kusaga viungo vya chakula (spice grinding machine) yenye uwezo wa kusaga 500 kg kwa saa, mashine ya kuchanganya viungo (spice mixing machine) yenye uwezo wa 1500 kg kwa saa, mashine ya kukaanga karanga (nuts roasting machine), mashine ya kufungasha na mashine ya kukaushia (packaging and solar drier).  Mkuu huyu aliomba SIDO Dar es salaam kupitia karakana zake,  kuzalisha mashine hizo tajwa kwa ajili ya kuvipatia na kuviwezesha vikundi husika.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo