Imewekwa: 16 Oct, 2025
Mafunzo ya kuongeza thamani mazao ya mboga mboga na mikunde yalifanyika katika Ofisi ya SIDO Manyara kwa kuwashirikisha Mama Lishe na Baba Lishe wa Mkoa wa Manyara. Dhumuni ni kubadili mazao ghafi kuwa bidhaa zenye ubora zaidi, muda mrefu wa kuhifadhiwa, na thamani kubwa sokoni. Washiriki walitoka katika Halmashauri zote za mkoa wa Manyara. Mafunzo yaliandaliwa kwa pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Ofisi ya SIDO Manyara na World Vegetable Center.

