MASHINE ZA UONGEZAJI THAMANI ZASHEHENI  BANDA LA SIDO
Imewekwa: 03 Jul, 2026
MASHINE ZA UONGEZAJI THAMANI ZASHEHENI  BANDA LA SIDO

Katika juhudi za kuendeleza viwanda vidogo na kuongeza ushindani wa bidhaa za ndani, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kupitia Vituo vya Kuendeleza Teknolojia (Technology Development Centres – TDCs) linaendelea kubuni na kuzalisha mashine mbalimbali za uongezaji thamani wa malighafi zinazotokana na sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

Wajasiriamali, wawekezaji na wananchi wote mnakaribishwa kutembelea Banda la SIDO katika Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2026.

Tembelea banda letu ujionee teknolojia za kisasa za usindikaji na uchakataji wa mazao, pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara. Pia utapata ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishaji, uendelezaji na uboreshaji wa viwanda vidogo na vya kati.

SIDO – Tunakuwezesha kuongeza thamani ya malighafi, kukuza biashara na kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo