KONGAMANO LA UENDELEZAJI WA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NA VIJANA LAFANYIKA TANGA
Imewekwa: 01 Sep, 2026
KONGAMANO LA UENDELEZAJI WA WAJASIRIAMALI WANAWAKE NA VIJANA LAFANYIKA TANGA

Kongamano la uendelezaji wa wajasiriamali wanawake na vijana limefanyika jijini Tanga tarehe 19 Agosti 2026 katika Ukumbi wa Tanga City, likiwa na lengo la kuwaunganisha wanawake na vijana na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo.

Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa wadau walioshiriki katika kongamano hilo. Kaimu Meneja wa SIDO Tanga, Bi. Gladness Foya, alishiriki katika jopo la majadiliano na kueleza fursa na huduma mbalimbali zinazotolewa na SIDO kwa vijana na wanawake.

Katika maelezo yake, Kaimu Meneja alitaja mafunzo ya ujasiriamali na stadi mbalimbali, huduma za ushauri wa biashara, uendelezaji wa bidhaa, matumizi ya teknolojia sahihi, pamoja na kuwaunganisha wajasiriamali na fursa za masoko na huduma nyingine zinazolenga kukuza biashara.

Wadau wengine walioshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na CRDB Bank, NMB Bank, VETA, pamoja na Idara za Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Maendeleo ya Vijana za Jiji la Tanga. Kongamano hilo pia liliambatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali wanawake na vijana.

Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, ambaye aliwakilishwa na Bi. Fatuma Kinyumbi, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii. Katika ujumbe wake, alisisitiza umuhimu wa wanawake na vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali na wadau mbalimbali ili kujenga biashara endelevu na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Mkoa wa Tanga.

Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya IMED kupitia programu ya Tanga Yetu, yenye lengo la kuwasaidia wanawake na vijana kuboresha biashara na bidhaa zao. Jumla ya wanawake na vijana 80 walishiriki katika kongamano

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo