Imewekwa: 19 Aug, 2025
Shirika la Kimataifa ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Vewanda Vidogo (SIDO) kwa pamoja wanatekeleza mradi wa nishati mbadala unaolenga kujenga uwezo wa kutummia amabaki ya mpunga ili kuzalisha mkaa mbadala kwa ajili ya nishati ya kupikia.
Warsha hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Mbeya na ilifungliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya Mh. Solomon Itunda ambae amesisitiza wananchi kushiriki katika fursa zinazojitoeza na kuletwa na wadau kama SIDO kwa ajili ya kujiletea maendeleo nchini. Aidha, Mkuu wa Wilay ameipongeza SIDO kwa mchango wake mkubwa katika kuleta meandeleo nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama UNIDO

