Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dr. Lusekelo Kasongwa na Dr. Enock Mwakalila (wa kwanza na wa pili kutoka kushoto), wametembelea ofisi za SIDO Mkoa wa Tanga kwa lengo la kujionea namna SIDO na CRDB Foundation zinavyoshirikiana katika kuwawezesha wajasiriamali vijana na wanawake kupata ruzuku kupitia mradi wa Green and Smart Cities.
Hadi sasa, jumla ya wajasiriamali vijana na wanawake 13 wamenufaika na ruzuku zenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 119,600,000. Aidha, maombi mapya ya wajasiriamali vijana na wanawake 46, yenye thamani ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania 350,000,000, tayari yamewasilishwa kwa ajili ya kuzingatiwa katika awamu ya pili ya utoaji wa ruzuku.
Ushirikiano huu unaendelea kuchochea ukuaji wa biashara za vijana na wanawake pamoja na kuimarisha mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa jamii.

