JUKWAA LA VIJANA LAZINDULIWA - MTWARA
Imewekwa: 03 Mar, 2026
JUKWAA LA VIJANA LAZINDULIWA - MTWARA

Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan moja ya ahadi zake ni kusaidia Vijana katika swala la uwezeshwaji kiuchumi. Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi Maendeleo ya Vijana,  Mh. Joel Arthur Nanauka na Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini anatekeleza hilo kupitia uanzishwaji wa majukwaa ya Vijana kila Mkoa.

 

Tarehe 2/03/2026, ilikua zamu ya Mtwara uzinduzi wa Jukwaa la Vijana.  Kupitia jukwaa hili serikali imetangaza fursa mbalimbali za uwezeshwaji vijana kiuchumi na moja ya fursa hizo ni kuitumia vizuri SIDO ili kuweza kuanzisha viwanda na miradi mbalimbali inayoweza kuongeza ajira kwa Vijana. SIDO Mtwara wakiwa ni moja ya watoa mada katika Jukwaa hilo, imeeleza mikakati mbalimbali Shirika iliyonayo katika utekelezaji wa sera na dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa kuzingatia maeneo muhimu ambayo ni uanzishwaji wa Viwanda vidogo vya uongezaji thamani mazao na huduma mbalimbali kwa Vijana;  kutoa mafunzo yanayoweza kuboresha mawazo ya biashara ili kuweza kupata miradi yenye tija;  kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya,  kutenga maeneo SIDO itaweza kuchochea uanzishwaji wa kongani ambapo vijana wengi wataweza kufanya shughuli zao kwa pamoja.

 

⁠Wizara ya Viwanda kupitia SIDO kwa kushirikiana na CRDB Foundation imetengewa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha vijana Tanzania nzima kwa ajili ya miradi ya Vijana kwa kuzingatia vigezo na masharti nafuu na wezeshi kabisa. Meneja wa SIDO Bi. Merina Mkuchu amewahimiza vijana Mkoani Mtwara kujiandaa kuzipokea fursa hizo kwa kuwa na miradi na mawazo bunifu kwa msaada wa ushauri wa Biashara kutoka SIDO Mtwara.  Ameongezea kuwa, anawakaribisha vijana wote  kufika  ofisi  SIDO Mtwara, kuzungumza na kushauriana ili maono na ndoto walizonazo ziweze kutimia.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo