VIJANA MKOANI KATAVI WAPATA MAFUNZO JUU YA USINDIKAJI WA NAFAKA
Imewekwa: 28 Jan, 2026
VIJANA MKOANI KATAVI WAPATA MAFUNZO JUU YA USINDIKAJI WA NAFAKA

Katika kutatua changamoto za ajira kwa vijana nchini, Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) imetoa mafunzo ya kuongeza thamani mazao ya nafaka  kwa Vijana 20 kutoka katika mkoa wa Katavi. Lengo ni kuwezesha washiriki hao kujiajiri na kuajiri vijana wengine kupitia miradi hiyo kwa kuongeza tija.

Mafunzo hayo yalifanyika katika Ofisi za SIDO Katavi kuanzia tarehe 16.01.2026 hadi tarehe 20.01.2026. Vijana hao walipatiwa ujuzi wa kuzalisha na kufungasha bidhaa zinazotokana na nafaka zikiwemo utengenezaji wa unga lishe, sembe, dona, kufungashaji wa mchele. Baada ya kupatiwa mafunzo hayo watawezeshwa kupata alama ya ubora kutoka TBS. Washiriki wa Mafunzo hayo walitoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Nsimbo na Tanganyika.

Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo