MASHINE ZA UONGEZAJI THAMANI ZASHEHENI BANDA LA SIDO
Katika juhudi za kuendeleza viwanda vidogo na kuongeza ushindani wa bidhaa za ndani, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kupitia Vituo vya Kuendeleza Teknolojia (Technology Development Centres – TDCs) linaendelea kubuni na kuzalisha mashine mbalimbali za uongezaji thamani wa malighafi zinazotokana na sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.

