img
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi, ametembelea Banda la SIDO katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF 2026) na kupongeza ushiriki mkubwa wa wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara. Katika ziara hiyo, ameeleza kufurahishwa na ubora na ubunifu wa bidhaa mbalimbali zinazooneshwa, hususan bidhaa zinazozalishwa na kusindikwa na vijana wajasiriamali. Ameipongeza SIDO kwa juhudi zake za kuwawezesha wajasiriamali kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo, na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwasaidia, hasa katika kuboresha vifungashio vya bidhaa ili viweze kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo