img
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) linawakaribisha wajasiriamali, wazalishaji, viwanda vidogo na vya kati, taasisi za Serikali, taasisi za fedha, mashirika ya maendeleo, kampuni binafsi, wabunifu, wavumbuzi na wadau mbalimbali wa sekta ya biashara na viwanda kushiriki katika Maonesho ya 5 ya SIDO Kitaifa 2026, yatakayofanyika katika Viwanja vya Magufuli Kahama, Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 21 hadi 30 Oktoba 2026. Maonesho haya yanatoa fursa ya kuonesha na kutangaza bidhaa, teknolojia na ubunifu; kupata masoko, wateja na fursa za uwekezaji; kunganisha wajasiriamali na taasisi za fedha na wadau wa biashara; kujifunza kuhusu teknolojia, uongezaji thamani na uboreshaji wa bidhaa na kujenga mitandao na fursa za ushirikiano wa kibiashara. USIKOSE FURSA YA KUONESHA, KUJIFUNZA NA KUFANYA BIASHARA! WOTE MNAKARIBISHWA
Matangazo
03 Dec, 2025
23 Nov, 2025
Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo