Kwa kutambua umuhimu wa wajasiriamali katika kujenga uchumi unaotegemea uzalishaji, ubunifu na matumizi ya fursa zilizopo ndani ya nchi, Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Mtwara limeendelea kujenga majukwaa yanayowaunganisha wajasiriamali na taasisi mbalimbali. Moja ya majukwaa hayo ni Siku ya Viwanda Mtwara, iliyowakutanisha zaidi ya wajasiriamali 150 kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na taasisi za Serikali, taasisi za fedha na wadau wa maendeleo.

