Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Tanga, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo, limeandaa kongamano la wanawake na vijana kwa lengo la kuwaunganisha na kuwafikishia taarifa kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika Mkoa wa Tanga.
Kongamano hilo limewaleta pamoja wanawake na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa, likilenga kuwajengea uelewa kuhusu fursa za kiuchumi, uwezeshaji, ujasiriamali na maendeleo ya biashara, pamoja na namna ya kuzifikia na kuzitumia fursa hizo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

