Ninayo furaha kuwakaribisha kutembelea tovuti ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO). SIDO ni muhimili muhimu wa Serikali katika kukuza na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati nchini kwa lengo la kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa na ustawi wa wananchi.
Huduma zinazotolewa na Shirika zinawawezesha wajasiriamali kujenga uwezo wao wa kuzalisha na kufungasha bidhaa zenye kukidhi viwango vya soko. Huduma hizo ni mafunzo na ushauri wa kibiashara; utengenezaji wa teknolojia zinazozalisha na kuchakata malighafi aina tofauti; masoko na uwekezaji; pamoja na huduma za mikopo.
Tovuti yetu ya www.sido.go.tz itakupa taarifa mbalimbali kuhusu ratiba za mafunzo na maonesho; matukio ya kijasiriamali; na mafanikio kutoka kwa baadhi ya wajasiriamali. Pia, tembelea katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii (sidotanzania) ili kuendelea kupata taarifa muhimu zitakazoendelea kukupa uelewa wa Shirika letu.
Karibuni sana!
Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji
Mkurugenzi Mkuu - SIDO

