Kukuza ubunifu
Ubunifu wa teknolojia ni mchakato ambao unawezesha upatikanaji wa teknolojia mpya au iliyoboreshwa na kusambazwa ili kuwafikia walengwa. Katika lugha fupi ubunifu wa teknolojia unahusisha utafiti, utengenezaji, ujalibishaji na usambazwaji wake kwa ajili ya matumizi. Viwanda vidogo na vya kati vinahitaji uboreshaji wa bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia teknolojia zilizoboreshwa. Watengenezaji wa tenolojia na Vituo vya SIDO vya uendelezaji wa teknolojia uwezeshwa na SIDO kwa njia mbalimbali ili teknolojia zilizoboreshwa ziweze kupatikana kwenye soko la ndani. Katika njia nyingine SIDO uwezesha mfumo wa ubunifu kwa njia ya vitamizi, makongano ya viwanda, n.k Teknolojia zote ambazo zimebuniwa na kuonyesha uboreshaji zinaonyeshwa kwenye 'Web portal' ili zifaamike na wahitaji waweze kuzipata.