Urasimishaji wa Biashara na Bidhaa

Taasisi nyingine za kisheria za biashara zinafanya kazi na SIDO ili kuweza kusaidia wajasiriamali , viwanda vidogo na vya kati kupata leseni,usajili na kurasimisha biashara.

Taasisi na makampuni mengi nchini Tanzania yanajiendesha nje ya mfumo wa sheria za biashara za serikali .Hali hii imesababisha taasisi na makampuni mengi ya biashara kushindwa kupata fursa na faida kutokana na vikwazo vya kutojiendesha kisheria.

Ili biashara, viwanda vidogo na vya kati viweze kukuza mitaji kwa kuanzisha au kukuza biashara zao vinahitaji kurasimisha biashara zao ili wamiliki wa biashara hizo waweze kupata fursa za kukuza  mitaji na fursa nyingine za kijamii na kiuchumi zilizopo katika kupanua masoko.

Baadhi ya taasisi hizo zinazoshirikiana na SIDO ni kama zifuatazo.

Mamlaka ya  Dawa na Vifaa Tiba  (TMDA)

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ni taasisi ya Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi

TMDA ambayo hapo awali ilikuwa ikijulikana kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2003. TFDA ilibadilishwa jina na kuwa TMDA mnamo tarehe 1 Julai 2019 kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi,
Sura 219 yaliyofanywa kupitia Sheria ya Fedha, Na. 8 ya mwaka 2019 ambapo udhibiti wa bidhaa za dawa ulitenganishwa na ule wa bidhaa za chakula.

DIRA
Kuwa Mamlaka inayoongoza katika kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa dawa,vifaa tiba,
vitendanishi na bidhaa nyingine za afya kwa wote.

DHIMA
Kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya dawa,
vifaa tiba vitendanishi na bidhaa nyingine za afya.

FALSAFA
Kutoa huduma bora za udhibiti katika kulinda afya ya jamii na mazingira kwa kutumia
wafanyakazi wenye ujuzi na ari ya kazi.

Mawasiliano

TMDA-Makao Makuu

P.O. Box 1253,

Dodoma or P.O. Box 77150, Dar es Salaam, Tanzania.

Telephone: +255 22 2450512 / 2450751 / 2452108

Nukushi: +255 22 2450793

Barua pepe: info@tmda.go.tz

Mamlaka ya Usajili wa Biashara na utoaji Leseni (BRELA)

Hii ni mamlaka iliyo chini ya wizara ya viwanda na biashara ,kwa dhumuni la kusimamia biashara na kuendesha sheria,kutoa usajili wa makampuni,usajili wa majina ya biashara,usajili wa biashara na nembo za kibiashara katika utoaji huduma, kutoa hati miliki na usajili wa viwanda . Ilianzishwa chini ya kifungu cha sheria namba 30 cha mwaka 1997 na kuanza utekelezaji wa kazi zake mnamo tarehe 3Disemba1999.

Mawasiliano

Brela

Eneo: Jengo la Ushirika Mnazi mmoja

S.L.P 9393,Dar es Salaam,Tanzania.

Simu namba: +255(0)222181344

Tovuti:www.brela.go.tz

Shirika la Viwango Tanzania

Shirika la viwango Tanzania (TBS) lilianzishwa chini ya wizara ya viwanda na biashara kwa sheria ya bunge ,sheria ya viwango namba 3 ya mwaka 1975 kama taasisi ya viwango ya taifa na kuanza kufanya kazi mnamo April 1976.Ilikuja kubadilishwa na kuitwa shirika la viwango Tanzania kwa sheria namba 1 ya mwaka 1977.Sheria ya viwango namba 3 ilikuja kubadilishwa badae na sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009,ambayo ililipa shirika nguvu zaidi katika uendeshaji wa kazi zake.

Shirika lilianzishwa kama jitihada ya serikali kuimarisha na kusaidia miundombinu ya viwanda na biashara kiuchumi zaidi.TBS ilipewa uwezo wa kupima na kudhibiti ubora wa bidhaa za aina zote na kuhamasisha viwango viwandani na kwenye biashara.

Mawasiliano

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Makao Makuu

Eneo : Eneo la Ubungo ,barabara ya Morogoro ya Sam Nujoma

S.L.P 9524,Dar es salaam,Tanzania.

Simu no:+255 222450298

Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA)

Chemba ya biashara na kilimo ilianzishwa mnamo mwaka 1988.Ilianzishwa chini ya msaada wa serikali ya Tanzania ili kuimarisha sekta binafsi.

Uanzishwaji wa TCCIA ilikuwa ni hatua nzuri ya kwenda katika uchumi ulio wazi,soko huria kwa sekta na mashamba yanayoendeshwa na watu binafsi.

TCCIA imefungua ofisi katika mikoa yote 21 ya Tanzania bara na zaidi ya vituo 90 katika wilaya mbalimbali ambavyo vinasaidia katika kuendesha shughuli zake.Ikisaidiwa na shirika la SIDA kutoka SWEDEN,TCCIA imeweza kuanzisha vituo katika mikoa na wilaya ,kutoa mafunzo,dhana za kiofisi na kukusanaya wafanyabiashara na kuwaongoza.

Vituo 21 vya TCCIA katika mikoa vinaunganisha sekta binafsi na serikali kwa dhumuni la kuvitangaza na maendeleo ya sekta binafsi.TCCIA inahamasisha serikali katika kuhudumia na kuhakikisha ukuaji na maendeleo ya sekta binafsi.

Mawasiliano

Tanzania Chamber of Commerce Industries and Agriculture(TCCIA)

Eneo:21 Mtaa wa Ghana

S.L.P 9713,Dar -Tz

Simu: +255-22-2119436

Tovuti:www.tccia.com

Tanzania Industrial Research and Development Organization(TIRDO)

Ni shirika linalojihusisha na utafiti pamoja na uendelezaji wa taasisi mbalimbali.Shirika hili lilianzishwa kwa sheria ya bunge namba 5 ya mwaka 1979 na likaanza utekelezaji mnamo tarehe 1 April 1979.Kazi yake kubwa ni kusaidia sekta ya viwanda Tanzania kwa kutoa utaalamu wa teknolojia na kusaidia katika kuboresha teknolojia zilizopo na zinazotumika, pia kufanya utafiti na kuongeza thamani ya malighafi zinazosindikwa kupitia viwanda.

Mawasiliano

TIRDO

Eneo : Kimweri

S.L.P 23235,Dar es Salaam,Tanzania.

Simu namba: +255-22-2666034

Tovuti : www.tirdo.org

Tanzania Private Sector Foundation(TPSF)

TPSF ilianzishwa chini ya sheria ya makampuni kifungu namba 212 mnamo tarehe 4 Novemba 1998.Ilianzishwa kama kampuni ili kuweza kuinua sekta binafsi kuweza kuwa mstari wa mbele katika masuala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania na lililenga kufanya shughuli zifuatazo:

                                                -Kusaidia taasisi wanachama kupata huduma wanazohitaji.

                                                -Kuelewesha na kuwasilisha lengo moja kusaidia sekta binafsi.

                                                -Kuihusisha serikali kama wakili mahsusi katika suala la kusaidia sekta binafsi.

TPSF ina nafasi ya kipekee katika sekta binafsi Tanzania kufanya shughuli mbalimbali ikiwa imelenga kuhakikisha mazingira mazuri ya biashara kwa sekta zote za kibiashara nchini Tanzania.TPSF inafanya shughuli zifuatazo ili kufikia malengo ya kutengeneza mazingira mazuri katika biashara.

                                          -Sera.

                                          -Uhusiano wa sekta binafsi na serikali.

                                          -Majadiliano ya kina.

                                          -Kuwasilisha mchango.

Mawasiliano

TPSF

Eneo: Mwaya Road,Msasani Peninsula.

S.L.P 11313,Dar es salaam,Tanzania.

Simu namba : 255 222601913

Tovuti:www.tpsftz.org

Mamlaka ya Uendelezaji wa Biashara Tanzania(TAN TRADE)

TAN TRADE ilianzishwa na sheria ya mamlaka ya uendelezaji wa biashara Tanzania namba 4 ya mwaka 2009.Kuanzishwa kwake kulifuatiwa na marekebisho ya sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1973 ambayo ilianzishwa na bodi ya nje ya biashara. TAN TRADE ina jukumu la kutekeleza sera ya taifa ya biashara ya ndani ya nchi na sheria ya bunge namba 5 ya mwaka 1978 ambayo ilianzishwa na bodi ya nje ya Biashara.

TAN TRADE ina jukumu la kutekeleza sera ya taifa ya biashara ,mkakati wa kuliwezesha taifa kufanya biashara za kimataifa (uuzaji wa bidhaa nje ya nchi), mahusiano ya kibiashara,sera ya masoko kwa ajili ya kilimo na sera ya sekta nyinginezo ili kutimiza lengo la kuendeleza biashara ya ndani na nje ya Tanzania.

Mawasiliano

TAN TRADE

 Eneo:Eneo la maonesho ya Sabasaba

 S.L.P 5402,Dar es salaam,Tanzania.

 Simu: 022 285023

 Tovuti: www.tantrade.go.tz

 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

 Mamlaka ya mapato Tanzania ilianzishwa na sheria ya bunge namba 11 ya mwaka 1995 na ilianza kufanya kazi zake mnamo tarehe 1 Julai 1996. Ili kuweza kufanikisha azma yake ,TRA inaendeshwa kwa sheria na jukumu lake ni kusimamia ukusanyaji wa kodi zote za serikali kuu.

Mawasiliano

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)

Eneo:Barabara ya Edward Sokoine,11105 Mchafukoge Ilala CBD.

S.L.P 11491,Dar es salaam,Tanzania.

Simu namba:

Tovuti:www.tra.go.tz

Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi(VETA)

Mamlaka ya mafunzo na ufundi stadi (VETA) ilianzishwa kwa sheria ya bunge namba 1 ya mwaka 1994,Ikiwa na jukumu la kuendesha ,kusimamia fedha za VET,kutangaza/hamasisha na kutoa elimu ya ufundi stadi na mafunzo kwa Tanzania.

Sheria mpya ya mafunzo ya ufundi stadi ilianzisha VETA iliyo na nguvu na mawanda mapana kama chombo ambacho kitazalisha soko lenye ajira  na ujuzi na kuweza kukusanya mapato kutoka makampuni tofauti.

Kazi za VETA

i.Kutoa fursa ya mafunzo ya ufundi stadi kwa mafunzo husika.

ii.Kuanzisha mafunzo ya ufundi yenye ubora katika mfumo wa biashara yenye kuhakikisha mahitaji yote yanafikiwa na sekta  rasmi na zisizo rasmi.

iii.Kuhamasisha mafunzo ya vitendo ili kuongeza ujuzi.

iv.Kuhamasisha uwiano wa usambazaji na uhitaji kwa wafanyakazi wenye ujuzi ili kuongeza kipato katika ajira na kwa uhitaji wa ujuzi ili kuwezesha watu kujiajiri katika maeneo ya vijiji na mijini.

v.Kuwezesha makundi mbalimbali kupata fursa za mafunzo hasa kwa makundi yasiyokuwa na uwezo wa kupata mafunzo hayo.

vi.Kuhakikisha upatikanaji wa mapato(fedha) kwa taasisi za mafunzo ya ufundi stadi.

vii.Kuongeza ubora na uzalishaji katika uchumi wa taifa.

Mawasiliano

VETA

Eneo:Chang'ombe Road,

S.L.P 2849, Dar es salaam,Tanzania.

Simu namba:+255 222863407

Tovuti:www.veta.go.tz

Taasisi ya Uwekezaji Tanzania(TIC)

Taasisi ya Uwekezaji Tanzania (TIC) ilianzishwa mnamo mwaka 1997 kwa sheria ya uwekezaji ya Tanzania kuwa mamlaka ya mwanzo kabisa ya serikali kuunganisha,kuhamasisha,kutangaza na kusisitiza uwekezaji nchini Tanzania na kuishauri serikali katika mambo yote ya sera ya uwekezaji na masuala yote yanayohusiana na uwekezaji. Mamlaka inahusika na biashara zote zilizowekeza nje ya nchi zisizozidi mtaji wa dola za kimarekani 300,000(USD)  na biashara zote zilizowekeza nchini zisizozidi mtaji wa dola za kimarekani 100,000(USD). Makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini na mafuta hasa petroli yanatakiwa kufuata utaratibu wa sheria kuthibitishwa.Hata hivyo mamlaka inasaidia wawekezaji kupata vibali , mamlaka n.k vinavyohitajika katika suala zima la uwekezaji Tanzania.

Mawasiliano

Taasisi ya Uwekezaji Tanzania

Sehemu:Shaaban Robert Street

S.L.P 938,Dar es Salaam,Tanzania.

Simu namba: +255(22)2116328-32

Tovuti:www.tic.go.tz

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

It appears your Web browser is not configured to display PDF files. Download adobe Acrobat