USHAURI,USIMAMIZI NA UELEKEZAJI

Katika uendeshaji wa biashara,wajasiriamali/wamiliki wa biashara mara nyingi hukumbana na changamoto ambazo mara nyingine huwa nje ya uwezo wao .Changamoto hizo huwalazimisha waweze kutafuta wataalam wenye ujuzi wa kutosha au wajasiriamali wenye mafanikio katika biashara na ujuzi zaidi ili waweze kuwashauri katika kupambana na changamoto hizo

Ushauri ni hatua ya kuweza kumsaidia mjasiriamali/mmiliki wa biashara ajitambue lakini pia kwa jina lingine ushauri huu waweza kuitwa uelekezaji. Mshauri humsaidia mteja kuweza kuzitambua changamoto,fursa , rasilimali, suluhu na kuchagua utendaji sahihi katika biashara.Hata hivyo wamiliki wa biashara ndogo hawawezi kugharamia kuwapata wataalamu wanaotoa huduma kibiashara.Lakini SIDO kiujumla ukiachilia mbali wafanyakazi wake, hutumia pia wajasiriamali wenye ujuzi na wenye mafanikio kuweza kuhamisha ujuzi wa kibiashara kutoka kwao na kuwasaidia wengine kwa mafanikio na uimara wa biashara zao.