BANDA LA SIDO, MAONESHO YA 48 YA SABASABA, 2024 LAVUTA WAONESHAJI WENGI

SIDO imeendelea kutoa huduma zake kwa wajasiriamali wadogo na wa kati  ikiwemo huduma ya masoko.  Kupitia maonesho yanayoandaliwa na SIDO na wadau mbalimbali bidhaa za wajasiriamali zimekuwa zinapata masoko  ndani na nje ya nchi.  Kwa mwaka huu 2024,  wajasiriamali  wapatao 135 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani  wameweza kushiriki katika Banda la SIDO kwenye maonesho ya 48 ya kibiashara Tanzania yanayojulikana kama  “Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam (DITF)” 2024.

Bidhaa ambazo zimeonyeshwa ni pamoja na bidhaa za  vyakula zilizo sindikwa, nguo, uhandisi, nguo, vipodozi na sabuni.  Pia watengenezaji na wasambazaji wa bidhaa za vifungashio wameshiriki ili kuonesha umahili na ubora wa vifungashio na ufungashaji wa bidhaa mbalimbali. Baadhi ya Kampuni za vifunganshio ni  Eco Consumers Ltd, Pet  Park Industries Limited, Mkepu, Vesha General Products Solution n.k.  Sambamba na ufungashaji huduma ya uchapishaji lebo zimetolewa kwa wajasiriamali waliohitaji kutoka kwenye kampuni ya DTP iliyobobea katika uchapaji wa vitu mbalimbali ikiwemo lebo. 

Maonesho haya ya 48 ya DITF ni fursa muhimu  kwa wajasiriamali wadogo na wa kati  kuweza kupanua wigo wa biashara ndani nan je ya nchi.  Pia ni jukwaa la kipekee la kuonyesha bidhaa zikiwemo za ndani ya nchi na kufanya mikataba ya biashara na kubadilisha maarifa na teknolojia.

Wajasiriamali wamepata pia fursa pia ya kukutana na sekta mbalimbali kama vile  kilimo, viwanda, ujenzi, teknolojia ya habari na mawasiliano, afya, elimu, na nyinginezo. Sambamba na kushiriki katika semina, warsha na mijadala inayohusiana na biashara  na maendeleo ya kiuchumi