BIDHAA ZA NGOZI

Swahili
Malengo: 
Mwisho wa program hii wahusika watakuwa na uwezo wa kuelewa namna ya kutengeneza na kuzalisha bidhaa za ngozi, uchaguzi wa vifaa na tabia za ngozi . Pia watakuwa na uwezo wa kutengeneza na kuzalisha bidhaa mbalimbali za ngozi kutoka kwenye ngozi zilizochakatwa na wao wenyewe.
Moduli: 
Jina la moduli: 
Bidhaa za ngozi na Uzalishaji wake
Maelezo ya Moduli: 
1.Maana ya ngozi (Ngozi mbaya na ngozi yenye ubora) 2.Uchaguzi wa vifaa . 3.Aina za mashine zinazotumika kwenye uchakataji wa ngozi . 4.zana na vifaa rahisi. 5.Uendeshaji wa cherehani. 6.Kutengeneza mikanda rahisi. 7.Kutengeneza folder za A4. 8.Kutengeneza mikoba ya kiofisi. 9.Utengenezaji wa waleti. 10. Utengenezaji wa mikoba ya shule. 11. Utengenezaji wa sendozi. 12. Utengenezaji wa viatu. 13. Kutengeneza vishikizo vya funguo za gari na makava ya simu.
Mbinu: 
Kujifunza kwa kushirikishana/mafunzo hayo yanaweza kufanyika kwa kiswahili au kiingereza,kazi za makundi,Uwasilishaji,kazi binafsi nk.
Kundi Husika Linalolengwa: 
Watu waliojifunza masuala ya uchakataji wa ngozi, watengeneza viatu na watu wanaojihusisha na ngozi.
Ada Ya Programu: 
TZS 300,000/= kwa muhusika (ada,chakula na steshonari)
Muda wa Kozi: 
wiki tatu