Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dr. Hashil T. Abdallah, akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya SIDO Mhandisi Musa Ally Nyamsingwa na Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Sylvester Mpanduji, walifanya ziara katika eneo la viwanda lililopo SIDO mkoa wa Dar Es Salaam. Pamoja na mambo mengine waliweza kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na wajasiriamali wapangaji katika maeneo hayo ikiwemo kiwanda cha kubangua korosho, kiwanda cha visaidizi mwendo kinachoendeshwa na walemavu (DAGE), kiwanda cha kuzalisha sabuni na vipodozi (STAR NATURAL), na kiwanda cha kutengeneza mita za maji za malipo ya awali kwa kutumia kadi au sarafu (SONAK).
Sambamba na ujio huo, Mheshimiwa Katibu Mkuu, aliweza kukutana na menejimenti ya SIDO ili kupata changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi.