Kilimo cha Uyoga

Ifuatayo ni orodha ya vitu vinavyohitajika kama unataka kuingia kwenye kilimo cha Uyoga: -

1. Vimeng'enywa.

2. Panga.

3. Nailoni la kutandika mezani.

4. Meza kubwa.

5. Mbegu ya Uyoga.

6. Banda la kuoteshea Uyoga.

7. Mifuko ya plastiki.

8. Pipa/Sufuria la kuchemshia vimeng'enywa.

9. Kamba ya kufungia mifuko.

10.Kichanja cha kuwekea vimeng'enywa baada ya kuchemshwa. Hiki hujengwa kwa kutumia fito au mianzi.

 

Jinsi ya kulima kilimo hiki lazima upate mafunzo ya Kilimo cha Uyoga.

Swahili
Malengo: 
Nia ya usambazaji wa elimu ya kilimo cha Uyoga ni: - 1. Kupata chakula bora kwa mwaka mzima bila kusubiri msimu wa mvua. 2. Ajira kwa akina Mama na Vijana kwani kinahitaji mtaji mdogo na mazao hupatikana katika muda mfupi. 3.Kujua matumizi rudia ya masalia ya uzalishaji. 4. Kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kutumia takataka. 5. Kupata uyoga wenye virutubisho muhimu. 6. Kupunguza matukio ya vifo vitokanavyo na kula uyoga wenye sumu.
Moduli: 
Jina la moduli: 
Kilimo cha Uyoga
Maelezo ya Moduli: 
Moduli ya Kilimo cha Uyoga inazo sehemu kuu tano: - 1. Kuandaa banda la kuoteshea Uyoga. 2. Matayarisho ya Vimeng'enywa, ikiwa ni pamoja na kuvichemsha. 3. Kuweka vvimeng'enywa kwenye mifuko ya plastiki. 4. Kupanda mbegu ya Uyoga kwenye mifuko ya plastiki. 5. Kuhifadhi mifuko iliyopandwa mbegu kwenye chumba cha giza kwa muda wa wiki 2 - 4, kisha itoe chumba cha giza na ining'inize kwenye shelfu ya miti.
Mbinu: 
Njia ya mafunzo ni ya ushirikishwaji pamoja na kujifunza kwa vitendo.
Kundi Husika Linalolengwa: 
Wakulima wapya wa kilimo cha Uyoga.
Ada Ya Programu: 
Shilingi za Kitanzania 150,000/= kwa kila mshiriki. ( Hii ni ada pamoja na steshonari)
Muda wa Kozi: 
Wiki mbili.