Swahili
SIDO chini ya ufadhili wa Serikali ya Korea ya Kusini, inajenga vituo viwili vya mafunzo ya usindikaji na uzalishaji wa vyakula katika mikoa ya Morogoro na Dar es salaam. Kazi ya ujenzi kwa sasa inaendelea, mashine na mitambo ya vituo hivyo imekwishanunuliwa na kupokelewa usimikaji utafanywa mara baada ya ujenzi kukamilika. Utoaji wa huduma katika vituo hivyo utaanza baada ya ujenzi wake kukamilika.