Mafunzo kwa Wakufunzi

Swahili

Washiriki wa Mafunzo ya TOT – Training of Trainers yaliyoandaliwa na SIDO. Washiriki walijifunza utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, nazo ni mvinyo, viungo mbalimbali, sausage, usindikaji maziwa, siagi ya karanga, juice ya matunda mbalimbali, sosi ya nyanya, pesti ya nyanya, na uokaji. Pia watajifunza utengenezaji wa sabuni za maji na miche, vipodozi.

Pia watapata mafunzo kutoka taasisi mbalimbali kama BRELA, TBS, TRA, OSHA, TMDA na wataalamu waliobobea katika sekta ya wajasiriamali. Lengo likiwa ni kuwaelimisha kuhusu taratibu mbalimbali za kusajili biashara/kiwanda cha usindikaji chakula, matunda, mbioga mboga na viungo; na utengenezaji sabuni na vipodozi.

PAMOJA TUJENGE VIWANDA