Mafunzo ya Usindikaji wa bidhaa kutokana na tunda la fenesi

Fenesi ni tunda kubwa linalopatikana Tanzania. Katika Tanzania linalimwa sana katika ukanda wa pwani. Fenesi linaweza kusindikwa bidhaa zaidi ya saba, na baadhi yao ni kama zifuatazo: -

1. Achali ya fenesi.

2. Jamu ya fenesi.

3. Juisi ya fenesi.

4. Wine ya fenesi.

5. Sirapu ya fenesi

6. Chips za fenesi.

7. Chokoleti za fenesi.

Swahili
Malengo: 
Kuwawezesha wasindikaji kujua bidhaa zinazoweza kusindikwa kutokana na fenesi, kujifunza njia za usindikaji wa bidhaa hizo na jinsi ya kuzifungasha. Kujua faida za kulitumia tunda la fenesi.
Moduli: 
Jina la moduli: 
Bidhaa zinazoweza kusindikwa kutokana na tunda la fenesi
Maelezo ya Moduli: 
1. Usafi na Usalama wa bidhaa za fenesi. 2. Udhibiti wa ubora wa bidhaa za fenesi. 3. Vifaa vitakiwavyo na visivyotakiwa katika usindikaji wa bidhaa za fenesi. 4. Mafunzo ya nadharia na vitendo ya usindikaji wa bidhaa za fenesi. 5. Ufungashaji wa bidhaa za fenesi. 6. Gharama na upangaji wa bei.
Mbinu: 
Njia ya mafunzo ni ya ushirikishwaji na kujifunza kwa vitendo.
Kundi Husika Linalolengwa: 
Wasindikaji wapya na waliopo kwenye sekta ya Usindikaji kwa muda mrefu.
Ada Ya Programu: 
TZS. 100,000/=
Muda wa Kozi: 
Wiki mbili