Meza ya cherehani

Swahili

Meza ya cherehani:

Hii ni meza inayotumiwa na mafundi wanaoshona nguo kwa kuweka cherehani juu yake ambayo inaendeshwa kwa kutumia mkanda unaozunguushwa kwa gurudumu linalosukumwa kwa miguu.

 

Meza hii inatengenezwa katika Mtaa wa Viwanda SIDO Tanga na fundi mmoja mjasiriamali aliyegharamiwa na TFSR CYMRU kusomea utengenezaji wa meza hizo katika chuo cha MSTC - SIDO Mwanza. Fundi huyu aliibadili na kutumia "bush" badala ya "bearing"

 

Jinsi ya kupata meza hii: -

Ili uweze kupata meza hii, unaweza kuwasiliana na fundi huyu kwa namba yake ya simu +255 762 424 123 / +255 659 424 123 au unaweza kuwasiliana na Afisa Ufundi - SIDO Tanga kwa namba +255 713 106 973.

Bidhaa: 
Meza ya cherehani
Mkoa: 
Tanga