MKOA WA MOROGORO

 

MAELEZO YA MKOA

Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa pili kwa ukubwa nchini ukitanguliwa na mkoa wa Tabora.  Mkoa una eneo la kilometa za mraba 73.039.  Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo la Tanzania Bara. kati ya eneo hili Km2 2,240 ni eneo la maji.  Mkoa umepakana na mikoa ya Pwani na Lindi kwa upande wa Mashariki, Manyara na Tanga kwa upande wa Kaskazini na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mikoa ya Dodoma na Iringa. Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Ruvuma.

Utawala:

Mkoa wa Morogoro kiutawala umegawanyika katika Wilaya sita ambazo ni Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga na Gairo.  Mkoa unao majimbo ya uchaguzi 10, Kata 212, Vijiji 673, Mitaa 295, Vitongoji 3,451.

Idadi ya watu:

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya kaya za Mkoa wa Morogoro ni 489,688 zenye watu 2,218,492 ambapo kati yao wanawake ni 1,125,190 na wanaume ni 1,093,302.  Wastani wa idadi ya watu katika Kaya ni 4.5.

Hali ya Hewa:

Mkoa hupata mvua mara mbili kwa mwaka.  Mvua za vuli hunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi katikati ya mwezi Januari, na mvua za masika hunyesha katikati ya mwezi Februari na kuishia mwezi Mei mwishoni.

 

 

 

 

Regional Profile: 
Contact
Mtu wa Kuwasiliana: 
Meneja wa Mkoa
Anuani: 
S.L.P 1022. Morogoro
Namba Ya Simu: 
0735103058
Simu Ya Mkononi: 
+255 767 265 295
Barua Pepe: 
morogoro@sido.go.tz