Mr. Renatus Chasuka anaisifu SIDO

RENATUS CHASUKA.
Ni mwanume mjasiriamali kutoka mkoa wa Rukwa ambaye anajishighulisha na Uhunzi. Alianza shughuli hii mwaka 1994 akiwa na msaidizi mmoja tu katika ofisi yake. Ni mteja wa mikopo katika Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO, alianza kukopa mwaka 2006 kwa kiwango cha chini cha Tzsh.200, 000/= kutoka katika mfuko wa NEDF. Mpaka sasa ameweza kufikia kiwango cha juu cha Tzsh.1, 000,000/= akiwa amekopa mara 6. Kutokana na kujiunga na mikopo ya SIDO amefanikiwa kukuza biashara yake kwa kubuni nyundo inayotumia umeme na kutoa ajira kwa watu wanne, Pia ameweza kujenga nyumba kubwa ambayo anaishi na familia yake.Vilevile kusomesha watoto wake kwa kuwalipia ada. Mjasiriamali huyu anaisifia SIDO na kuwataka wajasiriamali wengine wajiunge na SIDO kwani ni shirika zuri linalo wakopesha wajasiriamali kwa riba nafuu ya asilimia 18.

Swahili
Main Image: